Document Actions

Mfumo Badili wa Ukalimani (Alternative Interpretation System - ALIS)

Maombi ya uhimili wa kiteknolojia

Umuhimu wa mfumo badili za ukalimani ulijitokeza katika utaratibu wa vuguvugu la dunia dhidi ya utandawazi wa kipebari, iliyojumuisha maelfu ya watu kutoka kote ulimwenguni. Kuweko kwa wakalimani na vifaa mufti (vifaa vinafyosaidia wahadhiri kusikiliza wakalimani na pia wakalimani kusikilizana wenyewe) vikawa jambo la lazima katika kuandaa mikutano ya kimataifa kama vile Kumbi za Kimataifa.  Mtandao wa dunia wa wakalimani wa kujitolea (‘Babels’au mababeli) uliweza kutatua tatizo la kwanza. Katika kutatua tatizo la pili –vifaa mufti- suluhisho la kibiashara sio mwafaka, sababu mojawapo ikiwa bei kubwa, na nyingineyo ikiwa ni kwa minajili ya kuhimili juhudi mpya katika vuguvugu letu, kwa kutumia teknolojia inayokwepa mashirika ya kimataifa ya kibiashara.

Katika maandalizi ya awali ya Kumbi za Jamaa za Bara Ulaya na Dunia, kumekuwa na juhudi za kujaribu kuunda na kutumia mfumo badili wa ukalimani. Kwa misingi ya tajriba iliyokothili, kundi la ALIS, na ambalo lilianzishwa huko Ugiriki na wahamazishaji weye ujuzi wa kiteknolojia, limeunda mfumo huo kwa matumizi katika Ukumbi wa Bara Ulaya 2006 huko Athens. Mfumo huo ni wa kutegemewa, na unaweza kulinganishwa na ile ya kibiashara.  Umeundwa kwa misingi ya radio utangazaji wa radio wa FM, hivi kwamba wahadhiri wanaweza kusikiliza tafsiri kwa kutumia radio za kawaida. Zaidi ya hayo, mfumo huu unatumia Software ya Bure (Linux) kurekodi hotuba na tafsiri, kwa malengo ya kuhifadhi kumbukumbu za vuguvugu.  Huu ni mfumo ulio rahisi kutumia, "open-source", na nafuu.

Mfumo huu ni rasilimali muhimu kwa Kumbi za Kijamaa na utatumika Nairobi Januari 2007.  Huu ni mfumo ambapo bei ya vifaa ni kama sufuli.  Pia, unatoa uwezekano wa vikundi na mashirika katika vuguvugu kuandaa mikutano ya kimataifa yenye ukalimani wa moja kwa moja.. Mwisho, mfumo huu ni uvumbuzi wa kiteknolojia wa vuguvugu ambao ni kinyume na matakwa ya kisoko, ushahidi ingawa kwa kiwango kidogo, kuwa ulimwengu tofauti unawezekana,  ulimwengu usiotegemea faida.


Ikiwa una ujuzi wo wote wa kiteknolojia, unaweza kusaidia katika kuandaa UJD 2007 kwa kuhimili kiteknolojia mfumo ulioko wa ALIS.  Kwa habari zaidi/jinsi ya kushiriki katika ALIS, tembelea ukurasa wa mtandao www.babels.org/alis