Document Actions

faq

(Frequently Asked Questions) Kuhusu Ukumbi wa Jamaa Duniani 2007)

Yaliyomo

 

  1. Ukumbi wa Jamaa Duniani ni nini?
  2. Ukumbi wa Jamaa Duniani ulianza lini?
  3. Kumbi za Dunia za awali zilikuwa wapi na lini?
  4. Tarehe za UJD 2007 ni zipi? 
  5. UJD 7 itakuwa wapi?
  6. Kambi ya Kimataiffa ya Vijana itakuwa wapi?
  7. Ni nani anayetayarisha UJD 7
  8. Majukumu ya Kamati Andalizi ni yapi?
  9. Naweza kujitolea katika UJD 7?
  10. Kamati andalizi itashughulikia usafiri katika UJD 7?
  11. Kamati andalizi itashughulikia ushikamano na malazi badili katika UJD 7?
  12. Ni nani anayeza kushiriki katika UJD?
  13. Naweza kujisajilisha vipi katika UJD 2007?
  14. Ni nani anayesajili?
  15. Tendo la kibinafsi ni lipi?
  16. Nawezaje kuandaa jambo la kibinafsi?
  17. Tovuti ya moja kwa moja katika mtandao itakuwa tayari lini?
  18. Naweza kusajili wapi mambo ya kuwasilisha katika Ukumbi wa Nairobi 2007?
  19. Ni wapi ninakoweza kulipia ada ya kushiriki katika shughuli za Nairobi 2007?
  20. Je kutakuwa na vifaa vya ukalimani katika UJD 2007?
  21. Shughuli za sauti zinaweza kunakiliwa
  22. Naweza kuwasilianaje na sekretarieti ya Nairobi?

1. Ukumbi wa Jamaa Duniani ni nini?

Ukumbi wa Jamaa Duniani ni mahari wazi pa mikutano ambapo vuguvugu za kijamaa, mitandao, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, na mashirika mengine ya umma yanayopinga ukoloni mpya, na ulimwengu unaotawaliwa na upebari au na aina yo yote ya ubeberu hukusanyika ili kufuatilia fikra zao, kujadli maswala kwa njia za kidemokrasia, kuwashilisha mapendekezo, kubadilishana tajriba, na kutandawaza kwa ajili ya vitendo mahsusi.

Ukumbi wa Jamaa Duniani unasifika kwa ushirika wa watu tofauti na mambo kutoka kote duniani na hauhitaji kuungama, si wa kiserikali, au chama.  Unatafuta kuwezesha ushirikishi na utandawazi usiofungamana na mahali pamoja wa mashirika yanayohusika na utendaji halisi kutafuta ulimwengu mpya, katika kiwango cho chote kuanzia kile cha nyumbani hadi cha kimataifa, lakini hauna lengo la kuwa shirika linalosimamia jumuiya ya wahamashizaji duniani.

Ukumbi wa Jamaa Duniani sio kundi wala shirika.  Ni nafasi na pia utaratibu ambapo watendaji katika jumuiya ya wahamazishaji duniani huelezea ushikamano, wananufaika kutokana na vitendo vya pamoja, na kuendeleza ubunifu. Kwa habari zaidi, tembelea tovuti WSF Charter of principles.


2. Taratibu ya Ukumbi wa Jamaa Duniani ilianzaje?

Taratibu ya Ukumbi wa Jamaa Duniani ilianza mnamo 1998, ambapo pendekezo la Makubaliano ya Kimataifa Kuhusu Uwekezaji – katiba ya aina fulani ya rasilimali duniani ambayo ingeipa rasilimali haki zote bila majukumu, hasa katika ulimwengu wa tatu ambapo ‘uwekezaji’ ungefanyika- lilitangazwa.  Malalamiko yaliyotokana na upuuzi uliokuwa kwenye mkataba ule ulipelekea kuimbuka kwa vuguvugu la kijamaa la kupinga haya, jambo lililoifanya Ufaransa kujiondoa kutoka majadiliano yale mwishoni mwa 1998, na hatimaye kuzuia utiaji sahihi makubaliano hayo....

Kutokana na maingiliano yaliyozuliwa na matukio haya kila pahali baina ya wale waliokataa kukubali hali ya dunia ambayo inadhibitiwa na matakwa ya raslimali, aina tofauti za upinzani dhidi ya aina hii ya utandawazi yakaanza kujiunga.

Kwa muda wa takriban miaka ishirini, ‘wamilikaji wa dunia’ walikuwa wakikutana katika ukumbi waliouiota ‘Ukumbi wa Uchumi Duniani’, huko Davos, Uswisi. Mara moja kila mwaka, kundi hili hukusanya wote ambao wanaweza kulipia dala 20,000 za Kimarekani kusikiliza na kuzungumza na wasomi wakuu wanaotumikia raslimali. Mji wa Davos ndipo pahali ambapo nadharia ya utawala wa raslimali, katika mikakati ya ukoloni mpya, inaundwa na pole pole kutekelezwa.

 
Katika muktadha huu, Wabrazil kadhaa waliamua kuwa kulikuwa na uwezekano wa kuanzisha kiwango kipya cha upinzani dhidi ya mawazo haya  ambayo hadi sasa yanatawala ulimwengu.  Zaidi ya maandamano na malamiko ya umma, ilionekana kuna uwezekano wa kuendelea mbele na kutoa mapendekezo mahsusi, kutafuta suluhisho mwafaka kuhusu changamoto za kujenga ‘ulimwengu badili’, ulimwengu ambapo uchumi ungewatumikia watu wote, na si kinyume cha hiyo.  Fikra ilikuwa kwamba kupitia ushirikiano wa mashirika yote ambayo tayari yalikuwa yakishirikiana katika maandamano na  malalamiko, mipango ya mkutano tofauti wa dunia nzima ifanyike – Ukumbi wa Jamaa Duniani- uliolenga maswala ya kijamii.

Maandishi haya yamenukuu makala yalioandikwa na Francisco Whitaker, mmojawapo wa waanzilishi wa taratibu za UJD.  Waraka  wake wote unaweza kupatikana katika tovuti Brazilian World Social Forum website.

 

3. Ni wapi na lini ambapo UJD za awali zilifanyika?

  • UJD 2001 ilikuwa Porto Alegre, Brazil, kuanzia Januari 25 hadi 30. Walioshiriki walikuwa takriban watu 20,000.
  • UJD 2002 ilikuwa in Porto Alegre, Brazil, kuanzia Januari 31 hadi February 5. Walioshiriki walikuwa takriban watu 50,000.
  • UJD 2003 ilikuwa in Porto Alegre, Brazil, kuanzia Januari 23 hadi 28. Walioshiriki walikuwa takriban watu 100,000.
  • UJD 2004 ilikuwa Mumbai, India, kuanzia Januari 16 hadi 21. Walioshiriki walikuwa takriban watu115,000.
  • UJD 2005 ilikuwa Porto Alegre, Brazil, kuanzia Januari 26 hadi 31. Walioshiriki walikuwa takriban watu 155,000.
  • UJD 2006 ilikuwa imesambaa. Ilifanyika kwa njia ya kusambazwa duniani kama ifuatavyo:
    • Bamako, Mali, kuanzia Januari 19 hadi 23. Walioshiriki walikuwa takriban watu 25,000.
    • Caracas, Venezuela, kuanzia Januari 24 hadi 29. Walioshiriki walikuwa takriban watu 80,000.
    • Karachi, Pakistan, kuanzia Mechi 24 hadi 29.

Kwa habari zaidi, tembelea tovuti Brazilian World Social Forum website.

 

4. Tarehe za Ukumbi wa Jamaa 2007 ni zipi?

Tarehe za Ukumbi wa Jamaa 2007 zimetengwa kuwa Januari 20 hadi 25, 2007.

Siku za ukumbi zimepangwa kama ifuatavyo:

Jumamosi

Jan. 20, 2007

Sherehe za ufunguzi

Jumapili

Jan. 21, 2007

 

Siku ya kwanza (wazilisho za binafsi na za pamoja)

Jumatatu

 

Jan. 22, 2007

 

Siku ya pili (wazilisho za binafsi na za pamoja)

Jumanne

Jan. 23, 2007

Siku ya tatu (wazilisho za binafsi na za pamoja)

Jumatano

 

Jan, 2007

 

Siku ya nne (kupanga matukio ya 2007)

Alhamisi

Jan. 25, 2007

Sherehe za kufunga

 

5. UJD ya saba itakuwa wapi?

UJD ya saba itakuwa mjini Nairobi, Kenya. Mahali hasa pa tukio hilo patakuwa  Moi International Sports Centre  Kasarani – yapata kilomita 10 kaskazini magharibi mwa  ‘Central Business District’ ya Nairobi.  Sherehe za ufunguzi na kufunga zitakuwa huko Uhuru Park huko Nairobi.

 

6. Kampi ya Kimataifa ya Vijana itakuwa wapi?

Kampi ya Kimataifa ya Vijana itakuwa katika pahali hapo hapo kunako UJD - Moi International Sports Centre, Kasarani.

 

7. Ni nani anayepanga UJD 2007?

Ukumbi wa Jamaa 2007 inapangwa na Kamati Andalizi ya Afrika Mashariki (EAOC) na sekretarieti ya kamati hii ina makao yake mjini Nairobi, Kenya.  Kamati hii ina waakilishi kutoka Kumbi za Jamii Kenya, Uganda, Tanzania, Ethiopia na Somali.  Sekretarieti  hii imepewa makao katika Ukumbi wa Jamaa Kenya na Social Development Network (SODNET).

Tume saba zinajumuisha Kamati Andalizi:

    • Tume ya yaliyomo na mikakati;
    • Tume ya vyombo vya habari;
    • Tume ya kutafuta mtaji;
    • Tume ya mahali na mipango mingineo;
    • Tume ya vijana;
    • Tume ya mawasiliano na habari;
    • Tume ya uhamazishaji.

Kwa habari zaidi, tafadhari wasiliana na sekretarieti ya UJD 2007.

Kamati Andalizi ya Afrika mashariki hushughulika kwa ushiriakiano wa karibu sana na Baraza la Kimataifa, vikundi tekelezi, sekretarieti ya UJD mjini Sao Paolo, Brazil, Baraza la Ukumbi wa Jamaa Afrika na mashirika mengine ambazo zinafanya kazi katika Ukumbi wa Jamaa Ulaya.

 

8. Majukumu ya Kamati Andalizi ni yapi?

Kamati Andalizi ya UJD 2007 ina jukumu la kuhakikisha ufadhili bora wa kongamano hili la UJD jijini Nairobi.  Kamati hii inaendeshwa na watu na mashirika yaliyojitolea kufanikisha WSF Charter of principles, na pia kutoa ujuzi wao , wakati na mali kwa njia ya kujitolea.

 

9. Naweza kujitolea katika UJD?

Fomu ya kusijalisha kujitolea kuhudumu kwa ujuzi wao katika UJD inaweza kupatikana na wale wanaotaka katika tovuti hii.  Kujitolea kunaweza kuwa kwa njia nyingi tofauti – kwa mbali, katika mtandao, au kunako kazi, wakati na baada ya kongamano la Nairobi.

Kuna majukumu ya kitaalam na pia nafasi za jumla kwa watakaojitolea, na hizi zote zinapatikana katika tovuti ya nyumbani ya UJD 2007.

Tafadhali fahamu kwamba Kamati Andalizi ya Afrika Mashariki haitakuwa na uwezo wa kutoa nafasi yenye malipo kwa kazi za kujitolea.

Mara kwa mara, miito ya kujitolea kwa watu maalum kwa misingi ya ujuzi ama uegemevu kwa majukumu maalum itatolewa kwa tovuti ya nyumbani ya mtandao wa UJD 2007..

Ikiwa ungependa kujitolea katika utaratibu wa UJD 2007, unaombwa kuangalia  Call for volunteers yaani Mwito wa Kujitolea, na pia hakikisha kuwa umesoma Mikakati na Taratibu za Kujitolea ama Volunteer Policies and Procedures.

 

10.  Je, Kamati Andalizi itashughulikia maswala ya usafiri ya Kongamano la Nairobi?

Sekretarieti ya UJD 2007 haitawajibika katika kufanya mipango kwa mtu ye yote binafsi, vikundi ama mashirika.  Kila jumuiya ama watu waliosajiliwa kuhudhuria UJD 2007 itaandaa usafiri, malazi, bima, na mahitaji mengine.

 

11. Je, Kamati Andalizi itashughulikia mshikamano na malazi badili.

Kila mshiriki (waakilishi wa mashirika ama watu binafsi) atawajibika kwa malazi yake.

Sekretarieti ya UJD imechapisha orodha ya mikahawa jijini Nairobi.  Unaombwa kutembelea tovuti hii kwa habari zaidi.

http://wsf2007.org/info/hotel.xls

Eneo la kupigia kambi litakuwa tayari katika kampi maarufu ya Rowallan Camp inayopakana na Uwanja wa Maonyesho wa Jamhuri. Takriban watu 6,000 wanaweza kulala huko.  Kampi hii iko mwendo wa dakika 20 hadi 25 kwa basi kutoka eneo la UJD la Uhuru Park katikati mwa jiji la Nairobi.  Ili kupata habari za mapema, unaombwa kuwasiliana na sekretarieti ya UJD Nairobi.

 

12. Ni nani anayeweza kushiriki katika UJD?

Ushirika katika kongamano la Nairobi na katika utraratibu wote kwa jumla ni wazi kwa kila shirika, muungano au mtu binafsi ikiwa anakubaliana na kanuni za UJD yaani WSF Charter of principles.  Katika utaratibu wa UJD, ni mashirika pekee ambayo yanaweza kusajilisha na kuandaa maonyesho, ama yakiwa peke yake au kwa ushirika na mashirika mengine.

Wanachama wa vyama vya kisiasa au serikali za mitaa wanaweza kushiriki kama watu binafsi katika maeneo ya UJD2007 iwe ni katika kongamano lenyewe, au katika maeneo ya mtandao.

 

13. Naweza kujisajilisha vipi katika UJD2007?

Watu wote binafsi, mashirika, wanahabari, na waonyeshaji na wahudumu ambao wanahitaji vioski wanatakiwa kujisajilisha na kulipa ada ya usajili kama ilivyobainishwa na Kamati Andalizi ya Afrika Mashariki.

Kusajiliwa kwa watu binafsi.
Kusajiliwa kwa watu binafsi kwa UJD2007 kumefunguliwa.jijini Nairobi.  Ili kusajiliwa, unaombwa kunakili fomu yako ama Individual Registration Form kutoka kwa mtandao na kisha uitume kwa amwani registration@wsf2007.org.
Ilani maalum:  Anwani hii ya mtandao ni kwa MINAJILI TU ya kupokea fomu za usajili.

 
Siku chache baada ya kujisajilisha, utapokea namba ya siri au CODE inayohitajika ili uweze kulipia usajili wako binafsi, kisha utembelee tovuti ya kongamano (www.wsf2007.org) ili uweze kulipa kupitia mtandao.

Nambari hiyo ya siri ni muhimu kwa vile utahitaji kuitumia pamoja na idhibati ya chimbuko au “proof of origin”, katika meza ya usajili punde tu ukifika Nairobi hapo Januari mwakani.

Usajili wa maonyesho
Tafadhali unajulishwa kuwa utaratibu wa usajili kwa maonyesho utaanza yapata Oktoba ii, 2006.

Fomu za usajili
Maelezo kuhusu ada kadha wa kadha kwa watu binafsi, mashirika, maonyesho, vioski vya chakula, maonyesho au biashara zinapatikana kwa kunakili tovuti hii hapa here.

 

14. Ni nani anayesajilisha maonyesho?

Ni mashirika pekee yanayoweza kupendekeza maonyesho.  Tafadhali kumbuka kuwa maonyesho yanatayarishwa kibinafsi.

15. Onyesho la binafsi ni nini?

Onyesho la binafsi ni onyesho la aina fulani tofauti (kitamaduni, angavu, sherehekevu, jadilivu, tekelevu au kwa kimombo; cultural, demonstrative, celebrative, dialogical, practical ...) iliyoaandaliwa na kundi la ‘mashirika wenza’ (aina yo yote ya umoja) au shirika binafsi ambalo linashiriki na kukubaliana na utaratibu wa kumbi za jamaa duniani na kanuni za  WSF charter of principles.

Hii ina maana kuwa anayewasilisha maoni na mashirika wenzake atawajibika kwa utayarishaji, mipango, uandalizi na hatimaye kutekelezwa kwa onyesho lile wanalotaka kufanya katika kongamano la UJD2007 mjini Nairobi.

Hii pia inajumuisha kuleta au kununua mitambo na vifaa vinavyohitajika kama vile projekta, video, tanakilishi na kadhalika.

Kamati Andalizi ya Afrika Mashariki itaandaa nafasi ambapo maonyesho yatakuwa na pia vifaa vya ukalimani (sana sana).  Unaombwa kuhakikisha kuwa maonyesho yako yanasajiliwa mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili yawe katika ratiba ya kongamano la UJD2007 Nairobi.

 

16. Nitaandaa vipi onyesho la binafsi kwa ajili ya UJD?

UJD2007 imeshirikisha msururu wa mbinu ambazo zinahimiza matarisho ya mapema na pia vitendo sembamba zinazoelekeza maonyesho ya Nairobi.  Mambo haya yanayofuata na ambayo yametoholewa kutoka kwa  WSF consultation on actions, campaigns and struggles, na ambapo kumeafikiwa maegemeo ya kimanda yenye msingi katika maoni ya vuguvugu za kijamaa.  Baadhi yake ni:

    1. Kuujenga ulimwengu wenye amani, haki, maadili na heshima kwa nafsi tofauti;
    2. Kuufungua ulimwengu kutoka kwa utawala wa mashirika ya kimataifa na raslimali ya kifedha;
    3. Kuhakikisha upatikanaji wa kudumu kwa wote, wa bidhaa muhimu za kimaumbile na zilizoundwa na binadamu;
    4. Kuingiza demokrasia katika maarifa na habari;
    5. Kuhakikisha heshima, kulinda tofauti, kuhakikisha haki za jinsia na kuondoa kila aina ya ubaguzi;
    6. Kuhakikisha haki ya chakula, huduma za afya, elimu na kazi yenye utu;
    7. kujenga mfumo wa dunia kwa misingi ya mamlaka, uhuru wa uamuzi, na haki za watu;
    8. Kujenga uchumi wa kudumu wenye misingi ya watu;
    9. Kujenga taasisi na miundo ya kisiasa yenye demokrasia ya kweli kupitia kwa ushirika wa watu katika kufikia maamuzi na udhibiti wa masuala na mali ya umma;

17. Je, mtandao wa UJD utakuwa tayarii lini?

Uwanja wa kazi za mtandao za UJD unatarajiwa kuwa tayari manmo mwezi Oktoba.  Uwanja huu umetayarishwa ili kutoa uwezekano wa mashirika yenye mawazo sambamba kutayarisha na kuendeleza vitendo vitakavyoletwa katika kongamano la UJD, na kuvisajilisha katika ratiba ya Nairobi.  Uwanja huu unatoa vifaa vya kujumuisha kama vile orodha za anwani, uhariri na uchapishaji wa makala, nafasi ya habari, na eneo la uhifadhi..

Uwanja huu wa kazi unarahisisha usajili wa maonyesho iwe ni katika ngzi ya matayarisho au baada ya maandalizi pamopja na mashirika wenza.  Tafadhali tazama WSF Workspace presentation.

 

18. Naweza kusajili wapi maonyesho kaitika kongamano la Nairobi la Januari 2007?

Tovuti ya usajili itapatikana mwezi wa Oktoba katika uwanja wa kazi wa UJD2007.

19. Nitalipia wapi ada ya usajili kwa ajili ya kushiriki katika UJD2007?

Maingiliano ya usajili na malipo kwa jumla itapatikana Oktoba hii katika tovuti ya UJD2007 ili kurahisisha usajili na ulipaji wa ada kwa watu binafsi, mashirika na maonyesho kupitia mtandao.

Malipo yatakuwa kwa njia ya uhamishaji wa pesa katika benki na pia kutumia kadi za ‘credit’.  Habari kuhusu malipo kupitia benki itapatikana Oktoba.

Katika nchi mwenyeji Kenya, benki kadhaa zimearifiwa kupokea malipo ya usajili.  Habari zaidi kuhusu malipo haya zitapatikana katika mtandao mapema katika mwezi wa Oktoba.

 

20. Je, kutakuwa na vifaa na huduma za ukalimani?

Mababeli au Babels, mtandao wa wakalimani wa kujitolea, ni sehemu ya juhudi za kuandaa kongamano la  Nairobi na watakuwa na jukumu la kufanya ukalimani.  Alis, kundi la wataalam wa kujitolea linalofanya kazi na mababeli, litatoa sehemu kuu ya uhimili wa kiteknolojia kwa vifaa vya ukalimani.

Vifaa vya ukalimani vilivyofungwa vitakuwa vimewekwa katika vyumba kadhaa vya UJD2007 na jopo la wakalimani na vifaa vingine vitapatikana  vinapohitajika katika vyumba vinginevyo. Habari zaidi zitapatikana baadaye.

21. Je, matukio ya sauti yanaweza kunaswa kwa kanda?

Alis (kundi la Kigiriki ambalo lilivumbua vifaa badili vya ukalimani) imetayarisha software inayowezesha unakili wa matukio katika UJD.  Tanakilishi tembezi au hata ya ofisi inaweza kuunganishwa na mfumo wa matangazo katika vyumba vya maonyesho na hivyo kuwezesha unasaji wa kila sauti (tafsiri na lugha asili) 

Hiyo ni njia mojawapo ya kunakili yatakayojili.  Habari za kifundi zitapatikana baadaye katika tovuti za UJD2007.

 

22. Nawezaje kuwasiliana na sekretarieti ya UJD2007?

  • Makao makuu:

Masandukuni Lane, Off Vanga Road, Off Gitanga Road
S.L.P: 63125, 00619 Nairobi, Kenya
Simu: +254-(0)20-3860745 or +254-(0)20-3860746
Fax: +254-(0)20-2713262
E-mail: socialforum@sodnet.or.ke

  • Ofisi ya Dovenest:

Argwings Kodhek Grove, Off Argwings Kodhek Road
S.L.P. Box: 63125, 00619 Nairobi, Kenya
Simu: +254-(0)20-2713262 or +254-(0)20-2712646
Mobile: +254-(0)725 127 364