kuhusu UJD
Karibu na mnalikwa kuhudhiria Ukumbi wa Jamaa Duniani litalofanyika hapa Nairobi
Mkondo was saba wa WSF inayowanuganisha mashirika zisizo za serikali na vikundi mbalimbali kutoka nchi mbali mbali itafanyika mjini Nairobi, Mwezi January, tarehe ishirini hadi ishirini na tano. Mkusanyiko huo uta huthuriwa na watu takriban elfu themanini kutoka pembe zote za ulimwengu. Siku tano zimentengewa kusherekea na kushirikiana kwa utamaduni wa mkingamo kupitia warsha, utando, maandamano na mengineo.
Kutoka kianzilishi cha Ukumbi mwaka wa 2001 mjini Porto Alegre, fikira hii umekomaa na kubadilika kua pingamizi kuu duniana dhidi ya ubeberu na siasa yanaoambatana na ukoloni upya inyodhuru maisha ya watu na uchumi ya nchi za kusini, inayoimarisha madikteta, inayobagua vijana na wanawake, nyanyasa fukara duniani, adhiri mazingara na kuzua vita zisizo na maana.
Ukumbi, kupitia kilio cha “Dunia nyingine inawezekana”, umesisitiza umuhimu wa haki ya jamii, ushirikiano wa kimataifa, usawa wa jinsia, amani na kuitetea mazingara. Kutoka mji wa Porto Alegre, Mumbai, Bamako, Caracas, Karachi na sasa mji wa Nairobi, nguvu na genge ya Ukumbi wa Jamaa Duniani umepanua kwa pamoja, nafasi za demokrasi kwa manufaa ya wanaotafuta mbinu endelevu kama badili ya untandawazi mabepari.
Ukumbi wa Jamaa Duniani sio jaribo mpya ya kuunda nyendo ya mabadiliko.
Ukumbi pia, haina nia ya kuzipindua serikali tofaouti duniani. Fikira hii sio kikamilifu na haizingatii imani ya Mkataba wa Kanuni.
La, Ukumbi wa Jamma Dunia, tukitumia neno la Kiswahili, ni Jukwaa wa ulimwengu, au kwa neno nyingine, ni jukwaa wa kimataifa. Tukinukulu maana kutoka kwa Mkataba wa Porto Alegre, Ukumbi huu “ni nafasi wazi wa mkutano wa vikundi na nyendo ya jamii ya raia yanayoyapinga sheria za ukoloni upya na dunia uliotawaliwa na rasilmali au kupitia aina yeyote ya ubeberu. Lakini, vikundi hivi vitaunda jamii kikamilifu la haki ya binadamu, vikundi hivi vitajumuika kujadili fikra kidemokrasi, tunga mapendekezo, kubadilishana maarifa na kushirikiana kwa hatua mbalimbali”.
UJD Nairobi 2007 itakua fursa ya Afrika na vikundi vya jamii kuonyesha:
historia ya upingamizi dhidi ya utawala wa kigeni, ukoloni na ukoloni upya.
Afrika una utajiri wa mali, mila, lugha na makabila mengi;
Afrika na utamaduni wake wa kuwakaribisha na kuwakumbatia jumuiya toka nchi zingine ulimenguni;
Afrika na matoleo yake kwa ustaarabu wa ulimengu;
Afrika na jukumu lake la kuitafuta mabadiliko mpya na jamii changamfu duniani.
Anwani ya mkondo wa saba wa Ukumbi wa Jamaa Duniani ni “Misukosuko ya watu, Budi ya Watu.”
Maneno pekeyake haiwezi kuivundua ahadi na taharuki ya Ukumbi ijayo. Huna budi ila kuungana na washiriki na harakati zote: tutembea, kuimba, Kucheka, kucheza, kuoata, kushirikiana na mandugu na madada toka pembe zote ulimwenguni. (takriban nchi mia moja na arobaini).
Kwa hivyo, unaombwa kujiuinga nasi hapa mjini Nairobi, Afrika kutoka Januari 20 hadi Januari 25, 2007 tukiuumba upya mburuga ya Ukumbi wa Jamaa Duniani.
