Document Actions

Hati Ya Makubaliano (WSF)

HATI YA MAKUBALIANO

 

Kamati ya asasi za Brazil ambazo zilifikiria, na baadaye kuendesha, Jukwaa la kwanza la Jamii Staarabu la Dunia, ambalo lilifanyika Porto Alegre kuanzia tarehe 25 hadi 30 Januari, 2001, lilifanya tathmini ya matokeo na kuangalia hamasa iliyoamushwa na jukwaa hilo na kuona kuwa kuna umuhimu wa kuandaa hii Hati ya Makubaliano ili kuendeleza kazi ya mwitikio uliopatikana kwenye jukwaa hilo. Wakati vipengele vilivyoko kwenye Hati ya Makubaliano – vinapaswa kuheshimiwa na wote wanaotaka kushiriki kwenye Majukwaa yajayo ya Jamii Staarabu ya Dunia – huu ni mwendelezo wa maamuzi yote ambayo tayari yamefikiwa kwenye Jukwaa la Porto Alegre na ambayo yalikuwa ni chanzo cha mafanikio ya jukwaa hili, na ndiyo yatakuwa kiini cha shughuli nyingine za majukwaa yajayo.

 

  1. jukwaa la Jamii Staarabu la Dunia ni hadhara ya wazi kwa ajili ya kufanya tafakari ya kina, majadiliano ya kidemokrasia ya mawazo, uundaji wa misimamo, kubadilishana uzoefu kwa uwazi na kujongeana kwa ajili ya kuzipatia nguvu juhudi zetu, kwa vikundi na jamii ya raia staarabu, ambayo yanapinga uliberalli wa kisiasa na kutawaliwa na dunia ya kibepari na aina yoyote ya ubeberu, ambayo lengo lake ni ujenzi wa dunia kinayojali na kujenga mahusiano mema ya binadamu wote na binadamu na mazingira yake.

 

  1. Jukwaa la Jamii Staarabu ya Dunia lililofanyika Porto Alegre lilikuwa ni tukio ambalo lilitawaliwa na uzio wa muda na mahali lilipofanyika tukio hilo. Kuanzia sasa na kuendelea, na kwa kuzungatia ule ukweli uliojitokeza Porto Alegre kwamba “Dunia Nyingine Inawezekana” Jukwaa hili sasa linachukua sura ya mchakato wa kudumu wa kujaribu kujenga mikakati mbadala ambayo itaendeleza shughuli ambazo tayari zimeshaanzwa.

 

  1. Jukwaa la Jamii Staarabu la Dunia ni mchakato wa Dunia nzima. Mikutano yeyote ambayo itafanyika kama sehemu ya mchakato huu itachukua sura ya Kimataifa.

 

  1. Mikakati yote mibadala ambayo inapendekezwa kwenye Jukwaa la Jamii Starabu la Dunia inatofautiana kabisa/sana na mchakato waDunia ya Utandawazi unaoendelezwa na Makampuni ya Kimataifa na Serikali zake pamoja na Asasi za Kimataifa kwa maslai ya makampuni hayo, kwa kushirikiana na serikali za kitaifa. Vyombo hivyo vina dhamira ya kuhakikisha kwambaUtandawazi unakua ni hatua nyingine mpya katika historia ya Dunia. Madhumini ya Jamii staarabu ni kuhakikisha kwamba Haki za Binadamu zinaheshimiwa pamoja na zile za wananchi wote-za wanaume kwa wanawake-za Mataifa yote ikiwa ni pamoja na haki za kulinda mazingira yetu kwa demokrasia ya kweli ambayo italinda haki na usawa na uhuru wa mataifa wa kujitawala.

 

  1. Jukwaa la Jamii Staarabu la dunia linawaleta/linazileta pamoja taasisi na Jamii za kiraia kutoka nchi zote za Dunia,lakini jukwaa hili haliwezi kusema kwamba linawakilisha Jamii staarabu yote ya Dunia.

 

  1. Mikutano yote ya jukwaa hili haiwezi ikatoa maamuzi kwa niaba ya jamii staarabu kama chombo kinachojitegemea. Kwa hali hiyo basi, hakuna mtu atakaye ruhusiwa kutoa matamshi na msimamo akidai kwamba anatoa kwa niaba ya washiriki. Vivyo hivyo washuriki katika Jukwaa hawatatakiwa kutoa maamuzi, aidha kwa kupiga kura au kwa kutoa kauli ya ndiyo, kwa matamshi na misimamo inayoashiria kuchukua hatua, ambayo itawabana washiriki wote, au idadi ya kubwa ya washiriki, kwa kudai kuwa huu ndio msimamo wa Jukwaa kama chombo. Jukwaa hili sio  uzio wa madaraka wa kubishaniwa na washiriki kwenye mikutano, na jukwaa lisingependa kuwa ni njia pekee ya kutoa maamuzi ambayo yatawabana washiriki wake.

 

  1. Hata hivyo,taasisi au vikundi vya taasisi vinavyoshiriki kuwa kwenye mikutano ya Jukwaa hili wana haki, wakati washiriki wa mikutano hiyo kujadili kwa kina kuhusu hatua wanazozifikiria kuhusu  kuboresha shughuli za Jukwaa, aidha pekeyao au kwa kushirikiana na washiriki wengine. Ikitokea hivyo Jukwaa la Jamii Staarabu litajitahidi kusamabaza matamkona/au maamuzi hayo kwa wingi iwezekanavyo, bila ya kuongeza kuweka ukiritimba, bila ya kuzihariri au kuziweke vikwazo matamshi na misimamo hiyo, bali kuyasambaza kama yalivyo.

 

  1. Jukwaa la Jamii Staarabu la Dunia ni hadhara iliyowazi, isiyo na ubaguzi, isiyofungamana na Asasi zisizo za kiserikali au Vyama vya siasa, na ambayo haina mlundikano wa madaraka na ambayo inaunganisha taasisi na Asasi mbalimbali katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya jamii hadi kitaifa katika kujenga Dunia Mpya.

 

  1. Jukwaa la Jamii Staarabu la Dunia litabaki kuwa ni Jukwa la wazi ambalo litakubali ushiriki wa asasi na taasisi tofauti/mbalimbali kwa kuzingatia jinsia,makabila madogo,utamaduni,uwezo wa washiriki alimradi wanazingatia makubaliano yaliyomo kwenye Hati ya Makubaliano. Watu kutoka kwenye vyama vya kisiasa au vyombo vya ulinzi na usalama hawataruhusiwa kushiriki kwenye jukwaa hili. Viongozi wa serikali au wabunge/wawakilishi wanaokubaliana na mudhui ya hati hii ya makubaliano wanaweza wakaalikwa kushiriki kama watu binasfi.

 

  1. Jukwaa la Jamii Staarabu la Dunia linapinga vikali mawazo ya ukiritimba juu ya uchumi, maendeleo na historian a utumiaji wa nguvu za dola kama njia ya kudhibiti wananchi wao. Jukwaa linaheshimu haki za Binadamu, ujenzi wa demokrasia halisi na ushiriki, mahusiano mema na usawa ndani na kati ya watu, na Jukwaa linapinga aina yeyote ya ubaguzi na ukandamizaji wa mtu mmoja dhidi ya mwingine.

  1. Jukwaa ni mahala muafaka kwa kubadilishana mawazo mawazo kwa ajili ya kufanya tafakari ya haraka, na kusambaza matokeo ya tafakari hizo, kwa kuzingatia mbinu na mikakati inayotumika kutawala uchumi wa Dunia na kutoa mbinu na mikakati mbadala ya namna ya kuzuia kutawaliwa huko hasa ikizingatia kwamba ubepari huo unaambatana na ubaguzi wa rangi na jinsia na uharibifu mkubwa sana wa mazingira.

 

  1. Kama Jukwaa muafaka la kubadilishana uzoefu, Jukwaa hili linahitaji kuongeza maatano na uwelewano kati na ndani ya taasisi na asasi za kitaifa na kimataifa na jukwaa linathamini sana ubadilishanaji wa uzoefu huo, hasa zaidi katika kujenga chumi za nchi na uvumilivu wa kisisa katika kutimiza mahitaji ya wananchi na kutoharibu mazingira, kwaajiali ya kizazi cha sasa na vijavyo.

 

  1. Kama Jukwaa la ushirikiano, Jukwaa la Jamii Staarabu la Dunia linalenga katika kuimarisha na kujenga uhusiano mzuri kati ya taasisi na asasi za kitaifa na kimataifa ambazo kimtazamo zitajenga uwezo wa kupambana udhalilishaji (bila ya kutumia nguvu) wanaofanywa na utawala wan chi kwa watu wake. Aidha uwezo huo ni pamoja na kutengeneza mazingira mazuri yatakayoondoa udhalilishaji na unyanyasaji huo.

 

  1. Jukwaa la Jamii Staarabu la Dunia ni mchakato unaolenga kuhimiza taasisi na asasi shiriki kupanga mipango yake kwa kuzingatia hali halisi ya maeneo na nchi na kuomba ushirikiano wa kimataifa, kwani dunia hii ni yetu sote na sote ni wananchi wa dunia hii. Kwa hito basi, ni vizuri kupeleka kwenye ajenda ya dunia hatua njema zitakazosaidia katika kujenga dunia mpya.

 

IMEKUBALIWA NA KUPITISHWA SAO PAULO, BRAZIL, TAREHE 9 APRILI, 2001 NA TAASISI NA ASASI ZINAZOUNDA JUKWAA LA JAMII STRAARABU LA DUNIA.