Document Actions

Taarifa ya Usajili

Nairobi, Kenya, October 25th 2006

Kwa marafiki wa harakati za UJD,

 

Tuna furaha kuwajulisha kuwa usajili kwa toleo la saba la Ukumbi wa Jamaa Duniani, litakalo kuwa Nairobi Januari mwakani, ni wazi kwa watu binafsi, mashirika na amali au maonyesho.

 

Tafadhali kumbuka kuwa ni mashirika pekee – na wala si watu binafsi - yanayoweza kusajilisha amali/maonyesho

 

Tunakushauri kusajilisha mapema iwezekanavyo.We advise you to register as soon as possible.

 

 

  • Usajili wa kimashirika: usajili wa mashirika yaliyo na uwezo wa kutumia mtandao unafanyika katika www.wsfprocess.net. Mwongozo kamili kuhusu jinsi ya kusajilisha mashirika unapatikana hapo.  Kwa yale mashirika ambayo hayakuzoea mtandao, tumeambatanisha fomu ya usajili ambayo lazima itumwe kwa barua pepe kwa registration@wsf2007.org

 

  • Usajili wa amali/maonyesho: usajili wa amali/maonyesho pia unafanyika katika www.wsfprocess.net. Mwongozo kamili kuhusu jinsi ya kusajilisha amali/maonyesho unapatikana hapo. Kwa yale mashirika ambayo hayakuzoea mtandao, lakini yangependa kusajilisha amali/maonyesho katika kongamano la Nairobi, tumeambatanisha fomu ya usajili ambayo lazima itumwe kwa barua pepe kwa registration@wsf2007.org 

 

  • Habari muhimu: Fomu zote za usajili zinaweza kupatikana kutoka www.wsf2007.org. Tarehe ya mwisho ya usajili wa amali/maonyesho ni Novemba 30, 2006.

 

Kongamano la Ukumbi wa Jamaa Duniani Nairobi litatoa nafasi muhimu za ubunifu:  Siku ya nne (Januari 24) itatengwa kwa amali au maonyesho ya kibinafsi yanayoelezea mapambano, kupendekeza vitendo na kampeini za pamoja, kujenga ushirikiano wa karibu, na kubainisha ajenda za pamoja. 

 

Mwongozo kamili kuhusu jinsi ya kusajilisha amali/maonyesho katika siku ya nne unapatikana www.wsfprocess.net.

 

Katika tovuti ya kongamano la UJD 2007 jijini Nairobi - www.wsf2007.org. - utapata maelezo kuhusu jinsi ya kulipia mtu binafsi, shirika, na pia amali/onyesho.

 

Tunangoja kwa hamu kuu kukuona huko Nairobi kuanzia January 20 hadi 25, 2007.  

 

Katika mshikamano,

 

Prof. Edward Oyugi

Kamati Andalizi UJD 2007

 

Tazama: Uvumbuzi mwingine muhimu ni ule wa chombo cha usajili utakachotumia kusajili amali/maonyesho yaani (www.wsfprocess.net).  Kama utakavyogundua katika fomu za usajili, unaweza, ukitaka, kutumia fomu zizo hizo kusajilisha amali/maonyesho katika kongamanano nyinginezo fuatilizi baada ya Nairobi. Hiyo ndiyo maana chombo hicho kikaitwa wsfprocess.